Mtalaa huu wa Sukuma·Vuta kwa shule za mafunzo ya kilimo shambani (FFS) ni hatua kubwa katika kuingiza teknolojia ya Sukuma-Vuta katika mifumo ya utoaji ushauri kwa kilimo Afrika mashariki na kusini. Njia hii ya FFS inalenga kuwasaidia wakulima katika kuimarisha ubora wa teknolojia ya kusambaza na kuhakikisha wakulima wengi wananufaika kutokana na teknolojia bunifu. lngawa taasfsi za utafiti zimetayarisha teknolojia mseto za kutatua matatizo ya uzalishaji katika mifumo mingi ya kilimo katika mashamba madogo, uzalishaji katika kilimo umeendelea kushuka. Teknolojia nyingi hazijasambazwa vyema kwa sehemu kubwa ya wakulima na kwa hivyo kwa kiasi kikubwa hazijulikani ita tu katika sehemu ndogo ambapo zilifanyiwa majaribio. lsitoshe, nyingine hazijajaribiwa katika mashamba ya wakulima ili kutoa fursa kwa mabadiliko kuambatana na hali za maeneo husika. Mbinu zisizofaa za usimamizi na kuendelea kuongezeka kwa mzigo katika rasilimali, hasa rasilimali asili na rasilimali za kiuchumi kumezidisha hali hii.
Authors: Z. R. Khan, D. M. Amudavi, C. Midega, J. Pittchar, D. Nyagol, G. Genga, A. Ndiege, P. Akelo, J. A. Pickett, L. J. Wadhams, F. Muyekho and B. Nyateng
Contact address: zkhan@icipe.org
Institution: International Centre of Insect Physiology and Ecology (icipe)
Twitter name of the institution: @icipe
Twitter link: https://x.com/icipe
Available downloads: